Kwa picha.. kuhuisha usiku wa mwezi kumi na moja Muharam (usiku wa upweke)

Maoni katika picha
jioni ya Alkhamisi mwezi kumi Muharam 1443h sawa na tarehe (19 Agosti 2021m), limetoka kundi la waombolezaji waliokumbuka yaliyojiri kwa familia ya Hussein (a.s), baada ya kumalizika mapigano ya Twafu.

Wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika mkoa wa Karbala wamezowea kuomboleza usiku wa mwezi kumi na moja Muharam, unaojulikana kama usiku wa upweke (lailatul-wahsha), hukumbuka mateso waliyopata watu wa familia ya Imamu Hussein (a.s) kwa kufanywa mateka.

Waombolezaji huenda katika kaburi la mnyweshaji wenye kiu Karbala Abulfadhil Abbasi (a.s), kumpa pole na kumliwaza, kisha hukatisha katika uwanja wa katikati ya haram mbili na kwenda hadi kwenye malalo ya bwana wa mashahidi (a.s).

Katika matembezi hayo husomwa kaswida na tenzi za kuomboleza, aidha waombolezaji huwasha mishumaa katika uwanja wa katikati ya haram mbili, na jiraji ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: