Uwanja wa katikati ya haram mbili wasafishwa

Maoni katika picha
Kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili chini ya Atabatu Abbasiyya kinasafisha uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu na sehemu yenye paa pamoja na barabara zinazo elekea eneo hilo na maeneo yote yanayo zunguka sehemu hiyo, na kuondoa vifaa vyote vilivyo tumika wakati wa matembezi ya mazuwaru na yale ya towareji.

Kazi hiyo imeanza baada ya kumaliza ziara ya mwezi kumi Muharam, kitengo hicho kinafanya kazi ya kuhakikisha eneo hilo linarudi katika hali yake ya awali, usafi unaofanywa ni muendelezo wa usafi uliokua unafanywa wakati wa ziara.

Rais wa kitengo Sayyid Naafii Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Watumishi wa kitengo hiki kila msimu wa ziara hufanya kazi kubwa ya kuhudumia mazuwaru, matokeo ya kazi yao huonekana kwa mazuwaru kufanya ziara kwa amani na utulivu”

Akaongeza kuwa: “Pamoja na mazingira magumu kutokana na kuwepo kwa janga la virusi vya Korona, hakikua kikwazo katika kazi zetu, tumetoa kila aina ya huduma, kazi ya usafi imeenda sambamba na kupuliza dawa za kujikinga na maambukizi”.

Akafafanua kuwa: “Hatujaishia kufanya usafi peke yake, bali kunakazi za utangulizi kama vile kuondoa makapeti na nailoni aliyo kua imetandikwa chini ya kapeti, inayo kadiriwa kuwa na ukubwa wa mita elfu (15), pamoja na kuondoa vizuwizi vilivyo wekwa kwa ajili ya kuelekeza matembezi ya Towareji, na vitu vingine vilivyo wekwa kwa muda, tumesaidiwa na watu wa kujitolea katika kufanya kazi hii”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: