Maahadi ya Qur’ani tukufu imehitimisha vikao vya utafiti kuhusu misingi ya Qur’ani katika mapinduzi ya Imamu Hussein (a.s)

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa ya elimu ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia tawi lake la Baabil, imehitimisha vikao vya tafiti vilivyo fanywa chini ya anuani isemayo: (Uwelewa wa misingi ya Maisha baina ya mafundisho ya Qur’ani na mwenendo wa Husseini), chini ya uwezeshaji wa Dokta Haidari Shallaah, mmoja wa walimu wa kitivo cha masomo ya Qur’ani katika chuo kikuu cha Baabil.

Vikao hivyo vimefanyika katika malalo ya Sayyid Ahmadi Shawai (q.s) kwa kushirikiana na kamati ya vijana wa Ali Akbaru (a.s) hapa mkoani, vinalenga kuangazia mafundisho ya misingi ya Qur’ani iliyo tafsiriwa kwa vitendo na harakati ya Imamu Hussein (a.s), kwa kuangalia dalili tofauti na uwasilishaji wa mada kisasa.

Kumbuka kuwa Majmaa ya elimu ya Qur’ani, kupitia matawi ya Maahadi ya Qur’ani, hutoa mihadhara tofauti kuhusu vizito viwili, kwa lengo la kusambaza elimu itokanayo na chimbuko halisi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: