Hivi karibuni kituo cha masomo ya kimkakati kimetoa kitabu cha (sisi na mambo ya familia)

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha masomo ya kimkakati, chini ya kitengo cha Habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimechapisha kitabu cha (sisi na mambo ya familia) juzu la kwanza na la pili chini ya jopo la waandishi.

Juzu la kwanza limeandika historia ya familia katika utamaduni wa mashariki, sehemu ya kwanza inaeleza historia ya familia za Iraq (Rafidaini), familia za Misriyya za zamani, familia katika miji ya Farsi, familia za kale za wahindi, familia za wachina wa zamani, na sehemu ya pili imeandika historia ya familia za zamani za nchi za magharibi, na kulinganisha na familia za sasa.

Juzu la pili sehemu ya kwanza limeandika kuhusu utengenezaji wa familia katika uislamu, sehemu ya pili imeandika kuhusu malezi ya familia na sehemu ya tatu imeangazia changamoto za familia na namna ya kuzitatua.

Kumbuka kuwa kitabu hiki ni matunda ya kazi kubwa ya utafiti unaofanywa na kituo, tayari tumesha andika vitabu vingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: