Waliyyu-Damu ahutubia wauaji: Kwa macho gani mtamuangalia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w)?

Maoni katika picha
Imamu Zainul-Aabidina (a.s) katika siku kama hizi mwaka wa 61h, alisimama kwa ushujaa mbele ya twaghuti Ubaidullahi bun Ziyadi katika kikao chake akiwa ni mateka aliyefungwa minyororo, anamuangalia huku muovu huyo anachomba choma kwa fimbo yake mdomo wa baba yake, huzuni kubwa aliyokua nayo haikumzuwia kusimama na kukemea jambo hilo.

Hakika ushujaa alio onyesha Imamu Sajjaad (a.s) baada ya vita ya Karbala, akiwa mgonjwa tena mateka ni sawa na ushujaa wa katikati ya uwanja wa vita, alitoa hutuba maarufu iliyoliza watu wote waliokuwepo, kikawa kikao cha kwanza cha kuomboleza kifo cha Imamu Hussein (a.s) baada ya kuuawa kwake, Imamu aliongea mbele ya wauaji wa baba yake (a.s), imeandikwa na kitabu cha Arbaabu-Siirah na Almaqaatil:

(Kisha Zainul-Aabidina (a.s) aliwaambia watu nyamazeni, wakanyamaza. Akasimama, akamsifu Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.w) kisha akasema:

Enyi watu! Anayenijua basi ananijua, na asiyenijua: Mimi ni Ali bun Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s). Mimi ni mtoto wa aliyeuawa pembeni ya mto Furaat bila hatia wala kosa.

Mimi ni mtoto wa aliyevunjiwa heshima yake, na kuporwa neema zake, na kuchukuliwa mali zake, na kutekwa familia yake. Mimi ni mtoto wa aliyeuawa akiwa na subira, yatosha hiyo kuwa fahari. Enyi watu! Nakuambieni kwa utukufu wa Allah! Mnajua kuwa mlimuandikia baba yangu barua za kumwita na mmemhadaa? Mlimuahidi na kula kiapo cha utii kwake, mmevunja ahadi yenu na kumuua? Mmeangamia kwa mlicho kifanya, mmemchukiza Mola wenu. Kwa jicho gani mtamuangalia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) atakapo kuambieni mmeua kizazi changu, na mmevunja heshima yangu, nyie sio katika umma wangu?!

Akasema: Sauti za vilio zikawajuu kila upande, huku wakiambizana: Mmeangamia kwa mlichofanya. Akasema (a.s): Mwenyezi Mungu amrehemu atakaekubali nasaha yangu, na akatunza usia wangu kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na watu wa nyumbani kwake, hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu ni kigezo chema.

Wakasema wote kwa pamoja: Sisi wote ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu tumesikia, tumetii, tutahifadhi usia wako, hatutakuasi, tuamuru unachotaka -Allah akurehemu- hakika tutapambana na atakaepambana na wewe, na tutakua pamoja na atakaekupa amani, tutapambana na Yazidi! Na kujitenga na kila aliyekudhulumu na kutudhulumu.

Akasema (a.s): Iwe mbali! Iwe mbali! Enyi wenye visa na vitimbi, mmeponzwa na matamanio ya nafsi zenu! Mnataka kunidanganya kama mlivyo wadanganya wazazi wangu?!

Hapana huenda mcheza ngoma, hakika jeraha halijapona, baba yangu (a.s) ameuawa jana, na watu wa nyumbani kwake, sijasahau uzito wa msiba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu na uzito wa msiba wa baba yangu na ndugu zangu, uchungu wao umenijaa, maumivu yao yanatembea kifuani kwangu…).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: