Idara ya tahfiidh inaendelea kutoa mitihani kwa mahaafidh

Maoni katika picha
Itara ya tahfiidh katika Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaul-Ilmi Lilqur’anul-Karim, inaendelea kuwatahini wanafunzi waliohifadhi kitabu kitakatifu.

Mitihani hiyo ni sehemu ya malengo ya Maahadi ya kuendeleza mradi wa kuhifadhisha Qur’ani tukufu, ikiwa ni pamoja na mitihani endelevu kwa wanafunzi ili kukomaza uhifadhi wao na kuwafanya wajisomee zaidi walichohifadhi.

Tambua kuwa idara ya tahfiidh imeshafanya semina nyingi za ufundishaji wa Qur’ani na tahfiidh, wamesha hitimu makumi ya wanafunzi katika miaka ya nyuma, ambao wamehifadhi majuzu tofauti katika kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani ni kituo muhimu kwenye Majmaul-Ilmi Lilqur’anil-Karim katika Atabatu Abbasiyya, inalenga kusambaza elimu ya Qur’ani, na kuchangia katika kuandaa jamii ya wasomi wa Qur’ani katika sekta zote za maarifa ya Qur’ani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: