Sehemu ya historia ya Imamu Sajjaad ndio anuani ya mhadhara uliotolewa katika haram ya Ammi yake Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Kukumbuka na kuomboleza kifo cha Imamu Zainul-Aabidina (a.s), tawi lenye matunda katika mti wa Utume, mti wenye kivuli cha milele, asubuhi ya leo siku ya Ijumaa (25 Muharam 1443h) sawa na tarehe (3 Septemba 2021m), kulikua na mhadhara wa kidini ndani ya haram ya Atabatu Abbasiyya, katika ukumbi mtukufu wa Ammi yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Mzungumzaji alikua ni Shekh Muhammad Kuraitwi, anuani ya mada yake ilikua inasema: (machache kutoka kwenye historia ya Imamu Sajjaad a.s), akazungumzia sehemu za Maisha yake matukufu, hasusan baada ya tukio la Twafu na nafasi yake katika harakati za islahi, alizokuwa anaongoza baba yake bwana wa mashahidi (a.s), sambamba na kubakiza uhai wa harakati ya Husseiniyya.

Hali kadhalika akaongea kuhusu utukufu wake na karama zake (a.s), kama vile elimu, upole, ushujaa, msimamo, ukarimu, zuhudi na taqwa, na jinsi watu walivyokua wanampenda, na malezi mazuri aliyowapa wanachuoni waliojitolea Maisha yao katika kutumikia uislamu, na kazi kubwa aliyofanya ya kufundisha utamaduni wa kiislamu kwa kupitia dua zilizo kusanywa katika kitabu cha Sahifatus-Sajjadiyya na vinginevyo.

Majlisi imehudhuriwa na idadi kubwa ya mazuwaru na watumishi wa malalo hiyo takatifu, ikahitimishwa kwa kusoma kaswida na tenzi za kuomboleza zilizo amsha hisia za huzuni na majonzi ya kufiwa na Imamu wa nne, Imamu Sajjaad Ali bun Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: