Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Sistani anatuma salam za rambirambi kwa kufiwa na Sayyid Hakim

Maoni katika picha
Hii ni nakala ya rambirambi kutoka kwa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Sistani kufuatia kifo cha Faqihi wa Ahlulbait (a.s) Mheshimiwa Ayatullah Sayyid Muhammad Saidi Twabatwabai Alhakim:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu (Hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea)

Nimepokea kwa huzuni kubwa habari ya kifo cha Aalimu Rabani Faqihi wa Ahlulbait (a.s) Ayatullah Sayyid Muhammad Saidi Twabatwabai Alhakim (r.a).

Hauza ya elimu katika mji wa Najafu imepoteza nguzo muhimu, hakika alikua mtu aliyejitolea nafsi yake kwa ajili ya kunusuru Dini na madhehemu, Maisha yake yote aliyatumia katika kutumikia elimu na ameacha hazina kubwa ya elimu.

Natoa pole kwa Imamu wa zama (a.f) na hauza ya elimu, pamoja na familia ya marehemu na waislamu wote kwa ujumla, namuomba Mwenyezi Mungu mtukufu amuweke mahala pema peponi na amfufue pamoja na viongozi wake Mtume Muhammad na Aali wake watakatifu, na awape subira na uvumilivu familia yake na wapenzi wake, hakuna hila wala nguvu ispokua ya Mwenyezi Mungu mkuu.

Muharam/ 26/1443h

Ali Husseini Sistani
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: