Chuo kikuu cha Alkafeel kinaomboleza kifo cha Imamu Sajjaad (a.s)

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya, kimefanya maombolezo ya kifo cha Imamu Zainul-Aabidina (a.s), ndani ya ukumbi wake na kuhudhuriwa na makamo rais wa chuo katika sekta ya elimu na kundi la walimu na watumishi.

Majlisi ya kuomboleza ni sehemu ya harakati za chuo zinazo lenga kuangazia kumbukumbu za misiba ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s), katika kufanyia kazi kauli ya Imamu Jafari Swadiq (a.s) isemayo: (Huisheni mambo yetu, Mwenyezi Mungu amrehemu atakaehuisha mambo yetu), chuo kimekua kikifanyia kazi kauli hiyo tangu kilipo anzishwa katika kipindi cha mwaka mzima na kwenye kila tukio.

Majlisi ya uombolezaji ilifunguliwa kwa Qur’ani tukufu, iliyosomwa na msomaji kutoka Atabatu Alawiyya Sayyid Haani Mussawi, baada yake Shekh Jafari Waailiy akapanda mimbari, akazungumza kuhusu nafasi ya Imamu Sajjaad (a.s), katika kupambana na mmomonyoko wa maadili katika jamii baada ya vita ya Twafu na harakati ya baba yake (a.s), na jinsi waislamu walivyo amka baada ya kifo cha baba yake Imamu Hussein (a.s).

Aidha alizungumzia kazi kubwa iliyofanywa na Imamu Zainul-Aabidina (a.s), na nafasi yake kwa waislamu wote, namna alivyo walea kiroho na kuwafundisha uislamu sahihi, sambamba na kutaja vitabu rejea vinavyo aminika, aliendelea kufundisha imani na misingi ya Aqida.

Mwisho wa majlisi wahudhuriaji wakamuomba Mwenyezi Mungu ailinde Iraq na raia wake kwa baraka za Imamu Sajjaad (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: