Zaidi ya wanafunzi (100) wanashiriki warsha kuhusu mambo ya program katika chuo kikuu cha Alkafeel

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinaendesha warsha ya kielimu iliyoratibiwa na (Startup University) pamoja na (GDG Najaf) na kuhudhuriwa na Ustadh Ali Jaasim Al-Aamiriy mkuu wa kitivo cha uhandisi, kwa ushiriki wa zaidi ya wanafunzi (100) wa chuo kutoka ndani na nje ya mkoa wa Najafu.

Wamefundishwa kuhusu program za facebook na bwana Mustafa Tamimi, ameongea hatua muhimu kuhusu ufanyaji kazi wa program hiyo, kupitia uzowefu wake mwenyewe aliopata kwa mamia ya watu aliowafundisha namna ya kutumia mtandao wa facebook, aidha amefundisha mambo tofauti yanayosaidia na kujenga uwezo wa washiriki.

Akabainisha kuwa: “Maandalizi kwa ujumla ni mazuri na yanatia furaha, warsha ilikua nzuri sana, uongozi wa chuo umeweka kila kitu kinachohitajika katika kufanikisha warsha hii, kuanzia mpangilio wa ukaaji kati ya mtu na mtu pamoja na mambo mengine yote, tunaomba waendelee kuandaa warsha zingine katika siku zijazo, kwa lengo la kujenga uwezo wa wanafunzi wa chuo, na kuwafundisha namna ya kupambana na changamoto za maisha baada ya kuhitimu masomo yao”.

Mwisho wa warsha washiriki wameushukuru uongozi wa chuo kwa kuwaandalia warsha hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: