Kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel kimezindua mtandao maalum

Maoni katika picha
Kituo cha uzalishaji wa vipindi na matangazo mubashara Alkafeel chini ya kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefungua mtandao maalum kwa ajili ya kuonyesha matukia ya kidini yanayo fanywa ndani ya Ataba tukufu, miongoni mwa matukio hayo ni: (Filamu – taarifa za habari – picha za mnato – vipindi), sambamba na matangazo ya moja kwa moja ya matukio mbalimbali yanayo fanywa ndani ya Ataba, mtandao huo unaingizwa katika orodha ya mitandao ya toghuti ya kimataifa Alkafeel (toghuti maalum ya Atabatu Abbasiyya tukufu).

Mtandao huo unapatikana kwa anuani ya (Www.Alkafeel.tv) nayo ni zao la maendeleo ya kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel aidha ni sehemu ya kunufaika na maendeleo ya kimtandao, sambamba na juhudi zake za kuboresha sekta ya habari katika kila sekta.

Mtandao umetengenezwa kisasa zaidi na unakidhi mahitaji ya jamii na kuiweka karibu na Ataba tukufu.

Mtandao unamilango mingi, miongoni mwa milango hiyo ni:

  • - Maktaba ya picha za video: inapicha za video mbalimbali (filamu – program – ripoti – maelezo – khutuba za Ijumaa).
  • - Maktaba ya picha za mnato: inapicha za mnato tofauti, za Atabatu Abbasiyya tukufu na miradi yake, pamoja na ataba zingine na mazaru tukufu za ndani na nje ya Iraq.
  • - Matangazo mubashara: hurushwa mubashara saa zote eneo la hara na pembezoni mwake.

Kituo kimetangaza kuwa taasisi yeyote ya habari inayotaka kupata matangazo yenye viwango bora vya (HD) atume link yake kwenye namba ya simu (009647602402408) kupitia Whatssap au telegram, hiyo ni sehemu ya huduma inayo tolewa na kitengo cha habari cha Atabatu Abbasiyya tukufu kwa vyombo vyote vya habari bila kuchagua.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: