Tangazo la ratiba maalum ya kikao cha mada za kihauza katika kongamano kuhusu Imamu Hassan Almujtaba (a.s)

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la wanawake la nane kuhusu Imamu Hassan Almujtaba (a.s), imetangaza ratiba ya kikao cha mada za kihauza zitakazo wasilishwa kwenye kongamano hilo.

Kamati imesema kuwa majlisi itafanywa Jumapili ya kesho (4 Safar 1443h) sawa na tarehe (12 Septemba 2021m) katika chuo kikuu cha Baabil, itafunguliwa kwa kusoma surat Fat-ha kwa ajili ya kumrehemu Marjaa Dini mkuu Ayatullahi Udhuma Sayyid Muhammad Saidi Hakiim (q.s), kisha zitawasilishwa mada mbalimbali na wanachuoni tofauti, jumla ya mada 10 zitawasilishwa.

Tambua kuwa kongamano lilifanywa Alkhamisi iliyopita katika chuo kikuu cha Baabil chini ya anuani isemayo (Turathi za Imamu Hassan Almujtaba -a.s- katika masomo ya kibinaadamu, tafiti ya rai na rai nyingine).

Kumbuka kuwa kongamano husimamiwa na kamati kuu ya miradi ya Hilla mji wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), na idara kuu ya malezi katika mkoa wa Baabil na jumuiya ya kielimu Al-Ameed na chuo kikuu cha Alkafeel chini ya usimamizi wa uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: