Waziri wa mambo ya ndani katika ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu na amekutana na katibu mkuu

Maoni katika picha
Waziri wa mambo ya ndani Sayyid Othumani Ghanimi ametembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), asubuhi ya leo siku ya Jumapili (4 Safar 1443h) sawa na tarehe (12 Septemba 2021m), akiwa na kamanda wa kikosi cha Karbala pamoja na viongozi wengine wa idara ya ulinzi na usalama.

Baada ya kumaliza kufanya ibada ya ziara na kusoma dua mbele ya malalo takatifu, wamepokewa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Mhandisi Muhammad Ashiqar na baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo.

Katika kikao hicho katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya ameeleza maandalizi waliyo fanya kwa ajili ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), na hatua walizo chukua katika kuweka mazingira salama kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: