Atabatu Abbasiyya inafanya majlisi ya kuomboleza kifo cha Imamu Hassan Almujtaba (a.s)

Maoni katika picha
Idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wanafanya majlisi ya kuomboleza ndani ya haram ya Abbasi, katika kuhuisha kuuawa kishahidi kwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), Imamu wa pili na wanne katika watu wa (kisaa) shuka (a.s).

Majlisi imefunguliwa kwa Qur’ani tukufu, kisha akapanda mimbari Shekh Ali Zubaidi akaongea kuhusu historia ya Imamu Hassan (a.s), pamoja na upekee wake na yaliyotokea katika Maisha yake.

Ameeleza pia juhudi ya Imamu Hassan (a.s) katika kuthibitisha haki na kuonyesha batili, pamoja na matatizo aliyopitia katika maisha yake hadi kufikia kifo chake (a.s).

Majlisi ikahitimishwa kwa kaswida ya kuomboleza iliyo amsha huzuni katika nyoyo za waislamu wote walio hudhuria, kutokana na matatizo waliyopata watu wa nyumba ya Mtume (a.s).

Alifariki (a.s) mwezi saba Safar mwaka wa (50h), katika riwaya nyingine inasema mwezi ishirini na nane Safar (50h).

Kumbuka kuwa majlisi hii ni sehemu ya mradi wa Ummul-Banina (a.s) wa Tablighi za kidini, chini ya idara ya wahadhiri wa Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: