Atabatu Abbasiyya tukufu yajenga kituo cha kusafisha maji lita elfu 72 kwa siku

Maoni katika picha
Watumishi wa idara ya maji chini ya kitengo cha miradi ya Atabatu Abbasiyya wamekamilisha ujenzi wa kituo cha kusafisha maji (R.O station), kwa ajili ya kusambaza kwenye mji wa (Abu Zarnat) na mitaa ya Jirani na mji huo, kituo hicho kinauwezo wa kuzalisha lita elfu (72) kwa siku, kimejengwa ndani ya majengo ya Shekh Kuleini (r.a) chini ya Atabatu Abbasiyya.

Hiki ni moja ya vituo vingi vilivyo jengwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, ndani na nje ya mkoa wa Karbala, miji mingi iliyokua na tatizo la maji imenufaika na miradi hiyo, pamoja na mazuwaru.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara hiyo Mhandisi Basam Hashimiy kwa mtandao wa Alkafeel, amesema kuwa: “Ataba tukufu inazingatia sana ujenzi wa miradi ya kutoa huduma, na imesha jenga miradi mingi, miongoni mwa miradi hiyo ni vituo vya kusafisha maji (RO), tumesha jenga zaidi ya vituo (23) ndani na nje ya mkoa wa Karbala. Kikiwemo kituo hiki kitakacho hudumia idadi kubwa ya wakazi wa mji huu na maeneo ya Jirani, pamoja na mawakibu Husseiniyya na mazuwaru”.

Akasisitiza kuwa: “Kituo kinauwezo mzuri, mitambo yake yote imetengenezwa na makampuni bora na inauwezo mkubwa, hali kadhalika tumejenga mahodhi makubwa, kwa ajili ya kutunza maji”.

Aidha tumeongea na kiongozi wa majengo ya Shekh Kuleini Sayyid Ali Mahadi Swafi, amesema: “Tumekamilisha ujenzi wa kituo, na kuweka wasimamizi na waendeshaji wa kituo hicho, watakao linda maendeleo ya utendaji kazi kwa manufaa ya wananchi, waliokua na changamoto ya ukosefu wa maji safi ya kunywa, nao wameishukuru sana Atabatu Abbasiyya na wasimamizi wa mradi huu wa kibinaadamu”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imesha fanya miradi mingi ya kibinaadamu, ipo inayogusa maisha ya raia wa Iraq moja kwa moja, imefanya kila iwezalo kupunguza changamoto za wananchi, miongoni mwa changamoto kubwa ambayo imepewa kipaombele ni tatizo la ukosefu wa maji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: