Mazuwaru wamewasiri katika mpaka wa mji wa Samawa, na Ramithah yajitokeza kuwapokea

Maoni katika picha
Asilimia kubwa ya mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), waliotokea miji ya kusini mwa Iraq, mkoa wa Basra na mji wa Samawa wameanza kuwasiri katika mji wa Ramitha uliopo umbali wa (kilometa 25) kutoka makao makuu ya mkoa.

Ripota wa mtandao wa Alkafeel katika matembezi hayo amesema: “Miji yote inayopitiwa na mazuwaru katika mkoa wa Muthanna, kuanzia wilaya ya Hadhar hadi makao makuu ya mkoa wa Samawa, imekuwa mitupu ispokua maeneo machache, watu wa miji hiyo wameondoka kwenda kufanya ziara, baadhi ya watoa huduma kwenye mawakibu wamebaki wanaendelea na kazi huku wendine wakielekea Karbala au Baabil, kutoa huduma kwa mara nyingine”.

Akaongeza kuwa: “Watu wa Ramitha na mawakibu zao wamejiandaa kupokea mazuwaru wanao pita kwao, kutoka mkoa wa Basra na Naswiriyya na baadhi ya vitongoji vingine vilivyo ungana nao, wamekua wakishindana katika kuhudumia mazuwaru hao watukufu”.

Inabaki harakati ya wapenzi wa Imamu Hussein (a.s), hakika hali ya mapenzi yaliyojaa kwa mitume wa Mwenyezi Mungu, Imamu Hussein (a.s) akathibitisha misingi ya haki kwa kujitolea, alionyesha njia kwa damu yake takatifu, Imamu Swadiq (a.s) anasema: Haikuwa Dini ispokua mapenzi.

Hii ni sehemu ya picha zilizopigwa na kamera ya Alkafeel katika matembezi hayo wakati wakipita kwenye miji hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: