Mahaafidh wa Qur’ani tukufu wanashiriki katika kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani kwa mazuwaru katika mji wa Diwaniyya

Maoni katika picha
Vituo vya Qur’ani vilivyo funguliwa na Maahadi ya Qur’ani tukufu katika wilaya ya Shamiyya, vimeshuhudia ushiriki mkubwa wa wanafunzi wa mradi wa kuhifadhi kitabu cha Mwenyezi Mungu, wanatoa huduma ya ufundishaji wa Qur’ani kwa mazuwaru wanaoenda Karbala.

Mahaafidh hao wanashiriki kufundisha usomaji wa sura fupi na nyeradi za swala, Maahadi hutoa semina za ufundishaji bora wa Qur’ani kwa wakufunzi wake, sambamba na kuwashirikisha wanafunzi wanaohifadhi Qur’ani kwenye mradi huu ukizingatia kuwa asilimia kubwa ya wanufaika ni watu wenye umri mdogo.

Tambua kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu kupitia matawi yake mbalimbali inalenga kusambaza elimu ya Qur’ani na kuchangia katika kutengeneza jamii inayofanyia kazi mafundisho ya Qur’ani tukufu na yenye uwezo wa kufanya tafiti mbalimbali katika kila sekta inayo husu Qur’ani na fani zake.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu kila mwaka huhakikisha inatoa huduma nyingi zaidi kwa mazuwaru wa bwana wa mashahidi (a.s), ikiwa ni pamoja na ufundishaji wa Qur’ani tukufu unaoingia katika mkakati wa kutumikia vizito viwili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: