Huduma za kiibada.. App ya Haqibatu Mu-umin yahudumia zaairu wa Arubaini

Maoni katika picha
App ya Haqibatu Mu-umin, ni App muhimu katika Atabatu Abbasiyya iliyo tengenezwa na kitengo cha Habari- imefungua ukurasa wa kutoa huduma za kiibada katika ziara ya Arubaini, kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru na kusaidia sehemu ya mahitaji yao, wakati wa matembezi yao ya kwenda kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Msimamizi wa App hiyo bwana Ali Jiyashi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tangu kuanzishwa kwa App hii mwaka (2012m), wasimamizi wake wamekua wakiongeza kurasa na kuibiresha zaidi, kulingana na maendeleo ya sekta hiyo, hakika hii nyongeza ni sehemu ya mkakati wa App hii, kwani imekua ikifanyiwa maboresho daima na kuifanya kuwa App ya kisasa wakati wote, kuhusiana na ziara ya Arubaini na kwa ajiki ya kuchangia katika kuhudumia mazuwaru, tumeanza kufanyia kazi ukurasa huu kwa muda sasa, kwa kutoa huduma kupitia simuganja za kisasa”.

Akaongeza kuwa: “Ukurasa ulio ongezwa kwenye App na kupangiliwa kisasa ni kuhesabu kiwango alicho tembea:

  • - Zaairu anaweza kuhesabu idadi ya hatua alizo tembea na muda aliotumia, aidha anaweza kutoa sehemu ya matembezi yake na kumpa mtu yeyote amtakae sambamba na kufanya matembezi kwa niyaba.
  • - Muongozo wa zaairu (Google Maps): ni muongozo kamili ndani ya mkoa wa Karbala, unaonyesha anuani na majina ya:
  • 1- Sehemu muhimu.
  • 2- Mazaru na Ataba.
  • 3- Husseiniyyaat na misikiti.
  • 4-
  • 5- Mawakibu za kutoa huduma.
  • 6- Majengo yanayotoa huduma.
  • 7- Alama elekezi.
  • - Ziara ya Arubaini: nayo ni ziara maalum kwa Imamu Hussein (a.s).

Kumbuka kuwa App ya Haqibatu Mu-umin ni miongoni mwa Appa za kiislamu iliyokamilika, kutokana na taarifa za wachambuzi inazishinda App nyingi za mfano wake, hii inatokana na tafiti za kina zinazofanywa na wasimamizi wake, wameweza kutatua changamoto nyingi za wauslamu duniani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: