Atabatu Abbasiyya tukufu imeanza kutekeleza mkakati wa matibabu kwa ushiriki wa mamia ya madaktari

Maoni katika picha
Idara ya madaktari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeanza kutekeleza mkakati wake wa matibabu na kinga katika ziara ya Arubaini, ikiwa na mamia ya madaktari na wauguzi walio ajiriwa na wanaojitolea chini ya ushirikiano wa wizara ya afya ya Iraq.

Kiongozi wa idara Dokta Osama Abdulhussein ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Maandalizi ya jambo hili yalianza muda mrefu, chini ya maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu na idara yake, wametenga muda maalum kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru katika sekta ya afya”.

Akaongeza kuwa: “Mkakati uliandaliwa kupitia vikao mbalimbali vilivyo fanywa ndani ya ukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na katika maeneo yanayopitiwa na mazuwaru wengi wanapoenda Karbala, kama ifuatavyo:

 • - Tumefungua vituo viwili vya afya cha wanaume na wanawake ndani ya ukumbi wa haram tukufu.
 • - Kuandaa gari ndogo za wagonjwa, kwa ajili ya kubeba wagonjwa kutoka ndani ya ukumbi wa haram hadi kwenye vituo vya afya.
 • - Kuweka watoa huduma za kwanza wanaosaidia kuchukua wagonjwa na kuwapeleka kwenye vituo vya afya nje ya Ataba.
 • - Kufungua kituo maalum cha Ummul-Banina kwa ajili ya kupokea wagonjwa wa kiume nje ya haram tukufu.
 • - Kufungua kituo maalu cha Swidiqah Twahirah kwa ajili ya kupokea wagonjwa wa kike, vituo hivyo vipo karibu na mlango wa Imamu Haadi (a.s) Jirani na uwanja wa haram tukufu.
 • - Kufungua vituo viwili, kimoja cha wanaume na kingine cha wanawake karibu na mlango wa Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
 • - Kufungua hospitali karibu na mlango wa Bagdad iitwayo: (Hospitali ya Shahidi Wasaam Mussawi).
 • - Kufungua idara mbili za uokozi, moja ya ofisini na nyingine ya kutembea, kwa kushirikiana na idara ya kazi maalum.
 • - Kuweka gari za wagonjwa karibu na kila kituo cha afya, zenye vifaa tiba vyote muhimu kwa ajili ya kutoa huduma ya kwanza, na zilizo tayali kubeba wagonjwa na kuwapeleka kwenye hospitali za karibu.
 • - Kufungua vituo vya afya katika majengo yanayohudumia mazuwaru chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, upande wa Bagdad katika majengo ya Shekh Kuleini, upande wa Najafu katika mgahawa wa Ataba tukufu wa nje na kwenye maukibu ya Ummul-Banina (a.s), upande wa Baabil majengo ya Alqami, kwa kushirikiana na idara za afya za Diwaniyya, Misaan na idara ya afya ya Husseiniyya katika mji wa Karbala.
 • - Kufungua hospitali ya kisasa karibu na maukibu ya Ummul-Banina (a.s), kwa kushirikiana na idara ya afya ya Karbala na shirika la mwezi mwekundu la Iraq.
 • - Kuandaa jopo la madaktari maalum kwa ajili ya virusi vya Korona, kwa lengo la kuhudumia mgonjwa yeyote atakaedhaniwa kuwa na virusi vya Korona katika eneo la haram tukufu au karibu na haram, na kumpeleka kwe vituo maalim kwa ajili yao”.

Akabainisha kuwa: “Katika mkakati huu imeshiriki: “Idara ya Swidiqatu Twahirah ya madaktari – jumuiya ya Skaut ya Alkafeel – Idara ya mahusiano ya vyuo na shule – wataalamu wa Alkafeel wa uokozi na mafunzo ya udaktari – vitengo vingine kutoka ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, wizara ya afya na wizara ya ulinzi pamoja na sekta zingine”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: