Kitengo cha Dini kimetaja ratiba yake wakati wa ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetaja ratiba yake katika kipindi cha ziara ya Arubaini, yenye vipengele vingi vinavyo lenga kutoa huduma bora kwa mazuwaru katika sekta ya (Fiqhi – Aqida – Akhlaq – Malezi – Maelekezo), kutokana na Imani kuwa mada hizo ni miongoni kwa mambo anayotakiwa kuyafahamu zaairu na kunufaika nayo, sambamba na kunufaika na mazingira mazuri ya kiroho na kiibada yanayo patikana katika ziara hii tukufu.

Kwa mujibu wa maelezo ya makamo raisi wa kitengo hicho Shekh Aadil Wakiil, amesema: “Msimu wa ziara ya Arubaini ni miongoni mwa misimu ya kiibada ambayo zaairu mtukufu anatakiwa kunufaika nao, wahudumu wa kitengo chetu, Masayyid na Mashekhe wamebeba jukumu hilo, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu linavipengele vifuatavyo:

  • - Kufungua vituo vya maswali na majibu ndani na nje ya ukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kujibu maswali ya mazuwaru na kutoa ufafanuzi.
  • - Kutoa mihadhara ndani ya haram tukufu kuhusu ziara ya Arubaini na malengo yake.
  • - Kushiriki kwenye ratiba za kitablighi zinazo simamiwa na hauza ya Nafafu kwa kuhudhuria katika vituo vya tablighi na maelekezo.
  • - Kushiriki katika vituo vya kuhudumia mazuwaru vilivyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kujibu maswali na kutoa maelekezo kwa mazuwaru sambamba na kutoa mawaidha.
  • - Kuchapisha vipeperushi vya mafunzo tofauti na kuvigawa bure kwa mazuwaru”.

Akaendelea kusema: “Hali kadhalika tunatumia mitandao ya kijamii kupitia ukurasa wa maswali na majibu ya kisheria, pia wahudumu wanashiriki kwenye vipindi vya redio na luninga mbalimbali”.

Akamaliza kwa kusema: “Kila tulichosema kinafanywa pamoja na kazi za kila siku za kitengo, tunafanya kazi saa 12 kila siku”
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: