Idara ya Qur’ani imeanza kutekeleza ratiba yake ya ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Idara ya Qur’ani katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imeanza kutekeleza ratiba ya (sawa na Qur’ani tukufu) kwa ajili ya ziara tukufu ya Arubaini.

Ratiba hiyo inavipengele vingi vinavyo fanywa Atabatu Abbasiyya tukufu, ikiwa ni pamoja na mihadhara chini ya anuani isemayo: (Katika mapenzi ya Hussein -a.s- washindane wenye kushindana) yenye mada tofauti za Qur’ani, Akhlaq na Aqida.

Aidha ratiba hiyo inashughuli zinazo fanywa ndani ya ukumbi wa haram tukufu ya Abbasi, kusahihisha usomaji wa sura tukufu ya Alfat-ha, pamoja na kusoma Ayatu-Kursiyyu kwa mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Katika program hiyo, idara ya Qur’ani inagawa vipeperushi vinavyo elezea Qur’ani kwa mazuwaru watukufu, kama sehemu ya kuchangia kuwajenga kidini sambamba na kutoa huduma zote zinazo husiana na Qur’ani tukufu.

Kumbuka kuwa harakati za idara ya Qur’ani zinalenga kuinua kiwango cha wanawake kitamaduni na kifikra.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: