Baabil yaungana na baraka za matembezi na kuitikia wito wa Arubaini wa kuomboleza na kutoa huduma za Husseiniyya

Maoni katika picha
Kwa zaidi ya siku nne mji wa Baabil umekua ukishuhudia misafara mikubwa ya mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), na ndani ya siku mbili idadi ya watu wanaopita katika mji huo imeongezeka, asilimua kubwa ya watu wanaotoka katika mikoa ya kusini kama vile Basra, Naswiriyya, Misaan na Waasit wamefika katika mkoa huo.

Ripota wa mtandao wa Alkafeel katika misafara hiyo amesema: “Mazuwaru wameingia katika mji wa Hilla makao makuu ya mkoa wa Baabil kwa kupitia mipaka ya mkoa wa Diwania, ambapo wamegawanyika makundi mawili, moja limeelekea Najafu kwa kupitia barabara ya Kuful na lingine limeelekea Hilla, huku kundi linguine likipita katika mji wa Qassim (a.s), wataendelea na matembezi yao baada ya kumaliza kufanya ziara katika malalo tukufu ya Qassim (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Mji wa Hilla ni miongoni mwa malango makuu ya mazuwaru wanaoenda Karbala, barabara zote zimejaa mawakibu zilizo jiandaa kupokea mazuwaru wa Imamu Hussein (a.s) kutoka kila upande, mji wa Hilla ni mji wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s), hakika mji huo unaonyesha ukarimu wa mjukuu wa Mtume Imamu Hassan (a.s), kwa kuwapokea wageni wa malalo ya ndugu yake, wakazi wa mji huo wamejitokeza kwa wingi kuhudumia mazuwaru kwa kila wanacho hitaji”.

Akafafanua kuwa: “Mji wa Hilla ni miongoni mwa miji muhimu kutokana na kuwa karibu na mji wa Karbala, kila anayetaka kwenda kumzuru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka kusini mwa Iraq, lazima apite katika mji huo, hata akielekea barabara ya (Najafu – Karbala) akiwa anatoka kusini mwa Iraq, atapata barabara hiyo kwa kupitia katika lango la zamani la Hilla kwenye mkoa wa Diwaniyya, kama ilivyo kwa wanaoenda kumzuru Imamu Hussein (a.s) kwa kutembea, wanapo ingia katika mji wa Hilla hupata nguvu na ari hupanda kanakwamba wameingia katika mji wa Karbala”.

Sehemu ya picha za matembezi hayo…
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: