Kufungua kituo cha afya jirani na maukibu ya Ummul-Banina (a.s)

Maoni katika picha
Jirani na maukibu ya Ummul-Banina (a.s) chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefunguliwa kituo cha afya kinacho tembea (gari) lenye vifaa tiba muhimu vyote pamoja na dawa, kinasimamiwa na chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu kwa kushirikiana na jumuiya ya mwezi mwekundu ya Iraq, nayo ni sehemu ya maandalizi ya kiafya katika ziara ya Arubaini.

Makamo rais wa chuo katika mambo ya kiidara Dokta Alaa Mussawi amesema: “Chuo chetu kimekua kikijitahidi kutoa huduma bora kwa mazuwaru daima, sawa sawa iwe katika maukibu ya Ummul-Banina (a.s) ambayo ipo katika eneo letu au kutoa usaidizi kwa kila anayehudumia mazuwaru, pamoja na huduma za afya ambapo kituo hiki ni moja ya kielelezo cha wazi, kitatoa huduma za afya kwa mazuwaru wanaopita barabara ya (Najafu – Karbala)”.

Naye Ustadh Husaam Samiir mmoja wa madaktari wageni waliochini ya jumuiya ya mwezi mwekundu ya Iraq amesema: “Jumuiya kwa kushirikiana na wizara ya afya ya Iraq pamoja na jumuiya ya mwezi mwekundu ya Kuwait, tumeandaa gari hili lililojaa vifaa tiba mbalimbali, tuna mashine ya (CT scanner) na mashine ya (ultrasound) na mashine mbalimbali za vipimo vya damu, mapigo ya moyo, sukari..”.

Akamaliza kwa kusema: “Gari la kutoa huduma za afya linafuatana na magari mengine yaliyobeba vifaa tiba mbalimbali, vinavyo tuwezesha kutoa huduma ya matibabu, vavyo ni msaada kutoka nchi ya Kuwait, chini ya usimamizi wa wataalamu wa wizara ya afya na jumuiya ya mwezi mwekundu ya Iraq, na walimu wa kitivo cha uuguzi katika chuo kikuu cha Al-Amiid”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mwaka wa pili mfululizo, imekua ikiboresha huduma za afya katika vituo vyake vya kuhudumia mazuwaru wa Arubaini, idara ya madaktari imeweka mkakati maalum wa kuhakikisha wana toa huduma bora zaidi kwa kushirikiana na idara ya afya ya Karbala na sekta husika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: