Vituo vya kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani vyafungua milango yake katika mji wa Bagdad

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Bagdad chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, limefungua vituo vya kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani kwa mazuwaru wanaoenda Karbala kufanya ziara ya Arubaini, vituo hivyo vimewekwa kwenye vitongoji tofauti vya mji huo mkuu.

Vimepata muitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru na walimu wanajitahidi kuwahudumia, kwa kusahihisha makosa ya usomaji wa surat Fat-ha na sura fupi pamoja na nyeradi za swala.

Tambua kuwa tawi la maahadi katika mji wa Bagdad, kila mwaka hufanya harakati za Qur’ani bega kwa bega na matawi ya Maahadi ya mikoani.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa ya Qur’ani na matawi yake, huu ni mwaka wa tisa mfululizo inafanya mradi wa kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani kwa mazuwaru wa Arubaini, na inaendelea kutoa huduma za Qur’ani tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: