Swala ndefu zaidi ya jamaa katika barabara ya (Yaa Hussein)

Maoni katika picha
Barabara ya (Yaa Hussein) inayo unganisha mkoa wa Najafu na Karbala leo siku ya Jumamosi mwezi (17 Safar 1443h) sawa na tarehe (25 Septemba 2021m), imeswaliwa swala ya Dhuhuraini kwa jamaa ya mazuwaru wa Arubaini, iliyokuwa na urefu wa makumi ya kilometa, ikiwa na vituo kadhaa, kila kituo kimeswali jamaa kwa kuzingatia kanuni za afya, swala hiyo ni sehemu ya mradi wa Tablighi uliochini ya hauza.

Swala imeongozwa na mamia ya wanafunzi wa hauza kutoka Najafu mwaka huu, ilianzia katika nguzo namba (96) ilipo maukibu ya Atabatu Abbasiyya tukufu na ikaendelea kwa masafa marefu, miongoni mwa vituo vya swala hiyo ni maukibu ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, katika kituo hicho imamu wa swala alikua ni Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Ashukuuri, msimamizi mkuu wa mradi wa Tablighi za kihauza, hali kadhalika kulikua na swala ya jamaa katika mgahawa wa Atabatu Abbasiyya wa nje baada ya kukamilisha maandalizi yote ya swala hiyo.

Kwa mujibu wa watu walioshiriki kwenye swala hiyo wamesema kuwa inatoa ujumbe duniani, na inaonyesha imani ya wapenzi na wafuasi wa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) ikhlasi yao na umoja wao.

Ni ujumbe kutoka kwa watu wanaotembea kwenda kumzuru Imamu Hussein (a.s), usemao: Hatatukiwa na tabu kubwa, miguu kuvimba, vichwa kuuma, hakika hatuwezi kuacha kuswali, wala hatuswali ispokua katika wakati wake, swala ni nguzo ya Dini na sisi ni -Answaaru Hussein na mazuwaru wake- tunaosimamisha nguzo hiyo.

Kumbuka kuwa mradi wa Tablighi uliofanywa katika ziara za milioneyya zilizo pita, kwa kushirikiana na Ataba tukufu (Alawiyya, Husseiniyya, Kadhimiyya, Askariyya, Abbasiyya) ulifikia malengo tarajiwa ya kuingiza misingi ya Dini na Akhlaq katika nafsi za mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: