Ufunguzi wa kituo kikubwa cha kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu katika mji wa Baabil

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu tawi la Baabil chini ya Majmaa Qur’ani, imefungua kituo kikubwa cha kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani, chini ya mradi wa kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani kwa mazuwaru, jumla ya walimu 75 wanashiriki.

Kituo kinalenga kufundisha usomaji wa surat Fat-ha na sura fupi pamoja na nyeradi za swala, na kujibu maswali ya kiitikadi na kifiqhi, aidha kutakuwa na mashindano kuhusu maarifa ya Qur’ani na mambo ya kiimani, na program ya (Je unajua?) inayofafanua aya zinazo wahusu Ahlulbait (a.s), pamoja na kugawa vitambulisho vilivyo andikwa aya hizo, aidha vijana waliohifadhi Qur’ani tukufu watashiriki kuonyesha vipaji vyao kwa lengo la kuhamasisha vijana wenzao wafuate nyayo zao.

Kituo kinapokea maelfu ya mazuwaru wanaoenda Karbala, wanakuja kujifunza usomaji wa Qur’ani na masomo ya Aqida na Fiqhi, yanayo fundishwa na wasimamizi wa mradi huo katika mji wa Baabil.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Qur’ani tukufu chini ya Majmaa Qur’ani na matawi yake ya mikoani, inatoa huduma za Qur’ani katika mkoa wa Bagdad, Muthanna, Diwaniyya, Baabil, Hindiyya na Karbala, kupitia mradi wa kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani kwa mazuwaru, umepata muitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru na wamesifu huduma zinazo tolewa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: