Watumishi wa Majmaa Alqami wanahudumia mazuwaru wa Arubaini usimu na mchana

Maoni katika picha
Majmaa Alqami chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, inatoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru wa Arubani upande wa (Baabil – Karbala), wanaoenda kumzuru bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kiongozi wa Majmaa hiyo bwana Ali Ni’mah Khafaaji amesema: “Majmaa Alqami inatoa huduma tofauti kwa mazuwaru wa Arubaini kila mwaka, kuanzia tarehe kumi na mbili ya mwezi wa Safar, watumishi wa Majmaa huanza kugawa maelfu ya sahani za chakula (asubuhi, mchana na jioni), kila siku tunagawa zaidi ya sahani za chakula (15,000), kila tunapokaribia siku ya ziara zinaendelea kuongezeka”.

Akaongeza kuwa: “Huduma zetu haziishii kwenye kugawa chakula peke yake, tunakituo cha afya kikubwa kinachotoa huduma za matibabu kwa wanaume na wanawake, kwa kushirikiana na idara ya afya ya mji wa Diwaniyya, aidha tunavituo viwili, kimoja cha kuelekeza waliopotea na kingine cha kuwatambua watoto na wazee pamoja na watu wenye mahitaji maalum.

Akaendelea kusema: “Tunamchango upande wa elimu pia, tunakituo cha maelekezo ya kidini na kisheria, na kituo cha kufundisha usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu, aidha tunasehemu ya maonyesho ya kitaalamu yanayofanywa na kikosi cha Abbasi cha wapiganaji, wanaonyesha baadhi ya matukio yanayothibitisha ushujaa wa vijana wa fatwa takatifu ya kujilinda.

Kiongozi wa Majmaa akafafanua kuwa: “Tunasehemu za kupumzika na sehemu za kuswalia wanaume na wanawake, pamoja na sehemu ya vyoo kwa wanaume na wanawake”, akasema: “Maukibu inatoa huduma kwa mazuwaru saa 24 kila siku hadi tutakapo maliza msimu wa ziara”.

Kumbuka kuwa Majmaa Alqami ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na huhudumia mazuwaru kwenye kipindi cha ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), ipo katika barabara ya (Karbala – Baabil), inatoa huduma nyingi katika barabara hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: