Huduma mbalimbali zinazotolewa na Ataba mbili tukufu muda wote

Maoni katika picha
Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zinafanya kazi kubwa katika kuhudumia mazuwaru wa Arubaini kwenye barabara ya Najafu – Karbala, katika mgahawa wa Ataba mbili ambao ni kituo kikubwa cha mazuwaru wanaotumia barabara hiyo.

Mgahawa huo unatoa huduma mbalimbali kuanzia kugawa chakula, huduma za afya na huduma za maelekezo, kuna kituo kikubwa cha tabligh cha wanaume na wanawake, katika mgahawa huo pia kuna kituo cha ufundishaji wa usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu.

Mgahawa wa Ataba mbili unasehemu ya kupumzika na kulala mazuwaru pamoja na sehemu ya kulala wahudumu wa kujitolea na mubalighina, sehemu za kupumzika na kulala zimegawika sehemu mbili, upande wa wanaume na upande wa wanawake, hali kadhalika kuna sehemu ya vyoo na sehemu ya kuswalia.

Mgahawa umeshuhudia swala ya jamaa ndefu zaidi katika barabara ya (Yaa Hussein), mazuwaru wa Arubaini wameswali jamaa ya Dhuhuraini yenye urefu wa makumi ya kilometa, jamaa hiyo imeanzia katika mgahawa huo.

Mgahawa huo ni miongoni mwa vituo vya kwanza kutoa huduma, ulianza kuhudumia tangu zaairu wa kwanza kupita barabara hii ya Najafu – Karbala wanaoenda kwa baba wa watu huru (a.s).

Tambua kuwa mgahawa huu hutumiwa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika kuhudumia mazuwaru wa Arubaini, kupitia wahudumu wa Ataba hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: