Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu atembelea vituo vya kijana wa Alkafeel na kusifu huduma zinazotolewa

Maoni katika picha
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mhandisi Muhammad Ashiqar akiwa na wajumbe wa kamati kuu, ametembelea vituo vya kijana wa Alkafeel vinavyo undwa na wanafunzi wa chuo na shule za kawaida, chini ya uratibu wa idara ya mahusiano ya vyuo na shule katika kitengo cha mahusiano cha Ataba tukufu, program hii inafanywa kwa mwaka wa pili mfululizo kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru wa Arubaini.

Hii ni sehemu ya ziara zinazofanywa na katibu mkuu kwenye vituo vya kuhudumia mazuwaru vilivyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuangalia maandalizi waliyofanya kwa ajili ya kuhudumia mazuwaru wa Arubaini, zikiwemo huduma za kitamaduni zinazo tolewa na matawi (20), jumla ya vitengo nane vya Atabatu Abbasiyya vimeshiriki na vituo vingine vilivyo chini yake.

Katibu mkuu amesikiliza maelezo kuhusu huduma zinazo tolewa na kituo hicho kwa ujumla, kisha akasikiliza maelezo kutoka kwa kila tawi, akawapa maoni yake na maelekezo ya utekelezaji wa majukumu yao, aidha amesisitiza kufanya kazi kwa bidii na ustadi mkubwa kwa kiasi ambacho kinakidhi mahitaji ya mazuwaru, na waendeleze mafanikio ya huduma zinazo tolewa na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa mazuwaru.

Kumbuka kuwa kituo cha kijana wa Alkafeel kinaundwa na wanafunzi wa chuo na shule chini ya idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule kupitia kitengo cha mahusiano cha Atabatu Abbasiyya, kinashiriki kutoa huduma kwa mwaka wa pili mfululizo, huduma zake zimejikita katika mambo ya kitamaduni, hususan kwa tabaka la vijana, wameshiriki kupitia vitengo nane vya Atabatu Abbasiyya pamoja na vitengo vilivyo chini ya Ataba, wamegawika kwenye matawi ishirini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: