Ramani inayo onyesha sehemu muhimu zinazohudumia mazuwaru wa Arubaini na barabara za mji mtukufu wa Karbala

Maoni katika picha
Kituo cha Haqibatu-Mu-Umin chini ya kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetoa ramani inayo onyesha maeneo yote yanayohudumia mazuwaru wa Arubaini na barabara kuu na ndogo za mkoa wa Karbala, ramani hiyo inamrahisishia mtu kutambua kwa urahisi sehemu yeyote anayotaka kwenda.

Msimamizi wa kazi hiyo na kiongozi wa kituo Sayyid Ali Jayasi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hii ni moja ya huduma za kimtandao zinazotolewa katika ziara ya Arubaini, kupitia teknolojia ya simu ganja za kisasa”.

Akaongeza kuwa: “Ramani hii inasaidia zaidi watu wanaotembea kwa miguu na kila mtu anayetaka kujua ramani ya mji wa Karbala na maeneo muhimu ndani ya mji huo, nayo ni ramani ya kisasa zaidi katika mkoa wa Karbala, imeandikwa vizuri na inafahamika kwa urahisi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: