Kamera ya mtandao wa Alkafeel inakuletea picha za harakati za mazuwaru wa Arubaini katika siku ya Jumatatu, barabara zinazo elekea Karbala zimefurika mamilioni ya watu wanaotembea kwa miguu kwenda kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), picha zinaonyesha wazi wingi wa watu hao wanao hudumiwa na maelfu ya mawakibu katika barabara zote na kwenye kila kona.