Atabatu Abbasiyya tukufu: Idadi ya mazuwaru wa Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) imefika zaidi ya milioni 16

Maoni katika picha
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu baada ya Adhuhuri ya leo mwezi (20 Safar 1443h) sawa na tarehe (28 Septemba 2021m), umetoa tamko rasmi linalotaja idadi ya mazuwaru waliosajiliwa kupitia mfumo wa kuhesabu watu kielektronik, kuanzia mwezi 7 Safar hadi mwezi (20) imefika (16,327,542) milioni kumi na sita laki tatu na elfu ishirini na saba mia tano arubaini na mbili, walio ingia kupitia barabara kuu tano, ambazo ni: (Bagdad – Karbala), (Najafu – Karbala), (Baabil – Karbala), (Husseiniyya – Karbala) na Masaraini.

Ifuatayo ni nakala ya tamko hilo:

Tunatuma salam za rambirambi kwa Imamu wa zama Hujjat bun Hassan (a.f) na maraajii watukufu pamoja na ulimwengu wa kiislamu kwa ujumla, hususan taifa la Iraq ardhi ya mitume na mawasii, katika kumbukumbu ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu ailinde miji ya waislamu na kila baya, na awarudishe mazuwaru wa Abu Abdillahi Hussein (a.s) katika mataifa yao na miji yao wakiwa salama na wamekubaliwa ibada zao.

Kama kawaida kwa zaidi ya karne 13 mji wa Karbala umekua ikipokea mazuwaru wa bwana wa mashahidi Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), katika ziara ya Arubaini mwaka huu (1443h), watumishi wa Ataba wamepata utukufu wa kuwapokea na kuwahudumia mazuwaru watukufu, hakika Ataba imetoa huduma tofauti, ikiwemo huduma ya kuhesabu mazuwaru kwa kutumia mitambo ya kielektronik iliyo wekwe kwenye barabara kuu za kuingia katika mji wa Karbala, kupitia idara ya mawasiliano ya Atabatu Abbasiyya tukufu, huduma hii inatolewa kwa mwaka wa sita mfululizo, program hiyo imesimamiwa na kituo cha taaluma Alkafeel.

Idadi ya mazuwaru walioingia katika mji wa Karbala kuanzia mwezi (7 Safar) hadi saa 6:00 Adhuhuri ya mwezi (20 Safar) kwa mujibu wa mitambo ya kuhesabu watu kielektronik kupitia barabara kuu tano za: (Bagdad – Karbala/ Najafu – Karbala / Baabil – Karbala / Husseiniyya – Karbala / Masaraini) mwaka huu imefika (16,327,542) milioni kumi na sita laki tatu na ishirini na saba mia tano arubaini na mbili.

Idadi ya mazuwaru ndani ya miaka sita ya mwisho ilikua kama ifuatavyo:

  • 1- (16,327,542) milioni kumi na sita laki tatu na ishirini na saba mia tano arubaini na mbili, mwaka wa 1443 hijiriyya.
  • 2- (14,553,308) milioni kumi na nne laki tano na hamsini na tatu mia tatu na nane, mwaka 1442 hijiriyya.
  • 3- (15,229,955) milioni kumi na tano laki mbili na elfu ishirini na tisa mia tisa na hamsini na tano, mwaka 1441 hijiriyya.
  • 4- (15,322,949) milioni kumi na tano laki tatu na elfu ishirini na mbili mia tisa arubaini na tisa, mwaka 1440 hijiriyya.
  • 5- (13, 874,818) milioni kumi na tatu laki nane na elfu sabini na nne mia nane kumi na nane, mwaka 1439 hijiriyya.
  • 6- (11,210,367) milioni kumi na moja laki mbili na elfu kumu mia tatu sitini na saba, mwaka 1438 hijiriyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: