Gari za Atabatu Abbasiyya zimeanza kubeba mazuwaru wa Arubaini wanaorudi

Maoni katika picha
Mitengo cha usafirishaji katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza hatua ya pili ya kubeba mazuwari wa Arubaini, wanaotumia barabara ya (Karbala / Baabil) kupitia gari zaidi ya (300) zenye ukubwa tofauti.

Huu ni muendelezo wa hatua iliyoanza tangu mazuwaru walipo anza kumiminika kupitia barabara hiyo, gari zilizo pangwa kufanya kazi hiyo zinabeba mazuwaru kutoka Baabil hadi Karbala na Karbala Baabil.

Kazi hiyo itaendelea hadi zaairu wa mwisho, sambamba na vyombo vingine vinavyo shiriki katika kutekeleza ziara ya Arubaini, barabara hiyo hushuhudia msongamano mkubwa wa mazuwaru, ndio barabara inayo ingiza kiwango kikubwa cha mazuwaru.

Kitengo kimeunda kamati inayo simamia gari hizo na yenye jukumu la kutengeneza tatizo lolote litakalo jitokeza kwenye gari bila kwenda kwenye gereji za kitengo, sambamba na kupanga zamu ya madereva, ambapo kuna zamu mbili, asubuhi na jioni, umeanzishwa mtandao mbadala wa kusimamia gari hizo katika chumba cha ukaguzi, unaosimamia safari za gari hizo kuanzia karibu na kituo cha Ibrahimiyya, pamoja na kusimamia utiaji wa mafuta kwenye gari na matengenezo madogo madogo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: