Zaidi ya maukibu elfu 12 zimeshiriki kwenye msimu wa Arubaini mwaka huu

Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya bwana Riyadh Ni’mah Salmaan amesema kuwa: Idadi ya maukibu za Husseiniyya zilizo shiriki kwenye ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) mwaka huu imefika (12,400) zikiwemo maukibu (63) kutoka katika nchi za kiarabu na kiajemi, zilizo ingia ndani ya mipaka ya mkoa mtukufu wa Karbala na kusajiliwa rasmi.

Akaongeza kuwa: “Maukibu zilikua za aina tatu, za kutoa huduma ya chakula, vinywaji, kuandaa sehemu za kupumzika, sehemu za kulala na huduma zingine mbalimbali kwa mazuwaru, maukibu hizo zimejaa kwenye barabara zote zinazo elekea katika mji mtukufu wa Karbala zinazo tumiwa na mazuwaru, aina ya pili ni maukibu za kuomboleza, zinazofanya shughuli za uombolezaji (maukibu za matam na zanjiil), sehemu ya tatu inakusanya aina zote mbili (zinatoa huduma na kuomboleza)”.

Akafafanua kuwa: “Kitengo kilizikagua maukibu hizo na kuziwekea ratiba maalum, iliyotanguliwa na vikao kadhaa pamoja na wawakilishi wa maukibu hizo, kabla ya kuingia msimu wa Arubaini, kwa lengo la kuhakikisha zinatoa huduma nzuri zinazo endana na utukufu wa ziara hii, sambamba na kutatua changamoto zote”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: