Ziara ya Arubaini kwa niaba ya watu zaidi ya elfu 60.

Maoni katika picha
Idara ya teknolojia na taaluma za mitandao chini ya kitengo cha Habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imesema kuwa zaidi ya watu (60,271) wamefanyiwa ziara maalum ya Arubaini kwa niaba, kupitia ukurasa wa mtandao wa kimataifa Alkafeel (toghuti rasmi ya Atabatu Abbasiyya tukufu), kwenye toghuti zake za (Kiarabu – Kiengereza – Kifarsi – Kituruki – Kiurdu – Kifaransa – Kiswahili – Kijerumani), Pamoja na mitandao ya mawasiliano ya kijamii iliyo chini yake.

Kiongozi wa idara Ustadh Haidari Twalibu Abdul-Amiir amesema: “Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu ndio waliofanya ziara mbele ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuswali rakaa mbili pamoja na kusoma dua kwa niaba ya kila mtu aliyejisajili kwenye ukurasa wetu wa ziara kwaniaba”.

Akabainisha: “Asilimia kubwa ya watu waliojisajili wametoka katika nchi zifuatazo: (Iraq, Iran, Lebanon, Pakistani, Urusi, Marekani, Uingereza, India, Saudia, Swiden, Kanada, Kuawait, Malezia, Australia, Aljeria, Baharain, Afghanistan, Oman, Ekwado, Brazili, Ajentina, Uswisi, Naijeria, Ghana, Yemen, Indonesia, Italia, Hispania, Ufaransa, Uturuki, Adharbaijan, Qabrus, Finland, China, Ealend, Honkon, Japani, Falme za kiarabu, Sudani) pamoja na nchi zingine”.

Akamaliza kwa kusema: “Sasahivi tunajiandaa kufanya ziara kwa niaba kwenye kumbukumbu ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) mwezi (28) safar kupitia ukurasa huohuo kwenye mtandao wa Alkafeel”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: