Sehemu ya picha zilizopigwa na kamera ya Arubaini

Maoni katika picha
Ziara ya Arubaini ya mwaka huu imekua na ushiriki mkubwa wa vyombo vya habari vya ndani na nje ya taifa, ambavyo vimepiga makumi kwa maelfu ya picha, lakini -pamoja na wingi huo- havikuweza kuripoti ispokua sehemu ndogo ya misafara hiyo inayo hudhuriwa na mamilioni ya watu wanaomiminika katika mji mtukufu wa Karbala na kupokewa na Malaika waliopo katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili.

Wapigapicha wa kituo cha Alkafeel chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya wameshiriki kwenye misafara hiyo na kupiga picha tangu siku ya kwanza, waliweka utaratibu maalum wa kutekeleza jukumu lao.

Kazi yao ilipangwa kwenye vikosi tofauti, kulikua na kikosi cha nje kilicho tembea na mazuwaru wanaokuja Karbala, kikosi kingine kiliwekwa kwenye mipaka ya mkoa wa Karbala, kikosi kingine kikawa ndani ya mji wa Karbala na kingine ndani ya Ataba mbili takatifu Husseiniyya na Abbasiyya, picha zilizopigwa zimewekwa kwenye ukurasa maalum wa picha uliopo kwenye mtandao wa Alkafeel katika toghuti maalum.

Bila kusahau picha chache zinazo onyesha hisia za watu na kumbukumbu zao, hii ni sehemu ndogo ya picha zilizopigwa katika matembezi ya Arubaini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: