Ziara kwa niaba kwenye kumbukumbu ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika mji wa Madina na Najafu

Maoni katika picha
Idara ya teknolojia na taaluma ya mitandao chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza ziara kwa niaba ya kila mtu aliyepata udhuru wa kuja kufanya ziara kwenye kumbukumbu ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), ziara hiyo itafanywa ndani ya Raudha takatifu ya Mtume (s.a.w.w) pamoja na kwenye malalo ya wasii wake kiongozi wa waumini Ali (a.s), na kumpa pole kwa msiba huu mkubwa uliotokea mwezi ishirini na nane Safar mwaka wa (11) hijiriyya.

Watu wajisajili kwenye ukurasa wa ziara kwa niaba uliopo kwenye mtandao wa kimataifa kupitia link ifuatayo: https://alkafeel.net/zyara/.

Katika mji wa Madina ziara itafanywa Jirani na kaburi la Mtume kwenye msikiti wake mtukufu, itafanywa na kundi la waumini wa kujitolea miongoni mwa wakazi wa mji huo mtukufu.

Kuhusu ziara ya Najafu itafanywa katika malalo ya kiongozi wa waumini (a.s) kumpa pole kwa msiba huo, itafanywa na masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu, watakaoenda Atabatu Alawiyya siku ya mwezi ishirini na nane kufanya idaba hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: