Chuo kikuu Alkafeel kinaomboleza kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w)

Maoni katika picha
Chuo kikuu Alkafeel kinaomboleza kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), ndani ya ukumbi wa Shekh Tusi katika kitivo cha famasia, majlisi ya kuomboleza imehudhuriwa na rais wa chuo na wasaidizi wake wa sekta ya elimu na utawala, pamoja na viongozi, wakufunzi na watumishi wa chuo.

Majlisi ilikua na mhadhara uliotolewa na Sayyid Jafari Murawiji, amezungumza mambo mengi kuhusu mtukufu huyo, hauwezi kumuelezea kwa ukamilifu, ameongea kuhusu upekee wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) ukilinganisha na mitume wengine katika mambo mengi, miongoni mwa sifa za pekee kwake (s.a.w.w), yeye ni Mtume wa mshisho, Mwenyezi Mungu amempa hadhi ya kutotuma Mtume mwingine baada yake, hiyo inaonyesha ukamilifu wa ujumbe wake na kutokua na upungufu wowote, hali kadhalika upekee wa Qur’ani tukufu, kitabu kitakatifu cha Mwenyezi Mungu, na umma wake ndio umma bora, umeshuhudia utume wake na upweke wa Mwenyezi Mungu mtukufu.

Akaongea kuhusu mambo mengine, ikiwa ni pamoja na historia ya maisha matukufu yaliyojaa masomo, mazingatio, mawaidha na maadili, ambayo sisi kama waislamu tunatakiwa kuifanya kuwa dira na muongozo wa maadili yetu na vitendo vyetu, na namnagani alifanikiwa kumfanya mwanaadamu kuwa na huruma na mapenzi badala ya ukatili na chuku kwa kutumia upole wake na subira yake.

Kumbuka kuwa chuo kikuu Alkafeel kinazingatia kuhuisha matukio ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s), sawa yawe ya kuzaliwa au vifo, kwa kufanya mambo mbalimbali yanayo endana na aina ya kila tukio.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: