Ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu umehudhuria majlisi ya Arubaini ya Marjaa Dini mkuu Sayyid Muhammad Saidi Hakim (q.s).

Maoni katika picha
Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umehudhuria kwenye majlisi inayofanywa baada ya siku arubaini tangu alipofariki Aalimu mkubwa na faqihi wa Ahlulbait (a.s), Marjaa Dini mkuu Ayatullahi Sayyid Muhammad Saidi Hakim, iliyofanywa Masjidi Sahala jioni ya siku ya Jumanne (27 Safar 1443h) sawa na tarehe (5 Oktoba 2021m).

Ugeni huo umeongozwa na mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Jawadi Nasrawi, akiwa na baadhi ya watumishi wa malalo takatifu.

Ugeni huo umeipa pole familia ya Aali Hakiim kwa kuondokewa na Marjaa Dini mkuu (q.s), wakamuomba Mwenyezi Mungu mkuu amuweke mahala pemba peponi, na amfufue pamoja na babu zake watukufu, na awape umru mrefu wanachuoni wetu waliobaki.

Kumbuka kuwa Marjaa Dini mkuu Mheshimiwa Ayatullahi Sayyid Muhammad Saidi Hakim, aliyemaliza umri wake katika kusoma na kusomesha na kuutumikia uislamu na waislamu, alifariki siku ya Ijumaa mwezi ishirini na tano Muharam kwa maradhi ya moyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: