Maukibu ya chuo kikuu Alkafeel inahudumia mazuwaru wa malalo ya kiongozi wa waumini (a.s)

Maoni katika picha
Maukibu ya chuo kikuu Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inahudumia mazuwaru wa malalo ya kiongozi wa waumini Ali (a.s), waliokuja kumpa pole katika kumbukumbu ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w).

Rais wa chuo Dokta Nuris Dahani ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Maukibu ya chuo chetu inatoa huduma katika mkoa wa Najafu, kuhudumia mazuwaru hupewa umuhimu mkubwa na Atabatu Abbasiyya, tunashiriki kutoa huduma kwenye ziara tofauti zinazofanywa katika mkoa wa Najafu, ikiwemo ziara hii tukufu”.

Akabainisha kuwa: “Maukibu inaongozwa na watumishi wa chuo kikuu pamoja na wanafunzi wake, utawakuta wanashindana kuhudumia mazuwaru, maukibu inagawa chakula kila siku, pamoja na maji baridi ya kunywa na juisi, inatoa huduma siku zote za ziara”.

Kumbuka kuwa maukibu ya chuo kikuu cha Alkafeel, ilianzishwa sambamba na kuanzishwa kwa chuo hicho, na ikatumia jina la chuo, imekua ikipata maendeleo mwaka baada ya mwaka pamoja na kuporesha huduma zake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: