Watu wa Karbala wanampa pole kiongozi wa waumini katika kumbukumbu ya kifo cha Mtume (s.a.w.w)

Maoni katika picha
Watu wa Karbala kupitia maukibu yao ya uombolezaji, wamempa pole kiongozi wa waumini Ali (a.s), mbele ya malalo yake takatifu huko Najafu, katika kumbukumbu ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, zilizo jitolea usafiri na mambo mengine.

Rais wa kitengo hicho Bwana Riyadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Maukibu ya watu wa Karbala imezowea kuhuisha na kuadhimisha matukio tofauti ya watu wa nyumba ya Mtume (a.s) ndani na nje ya mkoa wa Karbala, ikiwa ni pamoja na tukio hili chungu, ambalo ni kilele cha misiba na majonzi, kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), maandalizi ya maombolezo haya yalianza zaidi ya siku tatu zilizopita, umewekwa utaratibu wa uombolezaji unaoendana na mazingira ya sasa”.

Akaongeza kuwa: “Maukibu imeingia usiku wa mwezi ishirini na nane Safar, inaundwa na vikundi tofauti vya watu wa Karbala, matembezi yake yalianzia katika Husseiniyya ya watu wa Karbala iliyopo Najafu, wakaelekea kwenye malalo ya mfiwa wa msiba huu Imamu Ali (a.s), na kufanya majlisi ya kuomboleza ndani ya malalo hiyo, wameimba kaswida mbalimbali na kusoma tenzi tofauti zilizo amsha hisia za huzuni na majonzi ya msiba huu”.

Akabainisha kuwa: “Watu wa Karbala wamezowea kufanya maombolezo haya, na siku ya pili baada ya kumaliza kuomboleza katika mkoa wa Najafu, huelekea kwenye malalo ya Imamu Qassim bun Mussa bun Jafari (a.s) katika mji wa Hilla, kwenda kuomboleza msiba huu mbele ya malalo yake takatifu”.

Akamaliza kwa kusema: “Maukibu itafanya matembezi ya kuomboleza pia kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Kumbuka kuwa maukibu ya kuomboleza ni utaratibu uliozoweleka kwa watu wa Karbala wa kuhuisha matukio ya Ahlulbait (a.s), maukibu hii inaudwa na vikundi tofauti vya watu wa mkoa mtukufu wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: