Kufungua vituo vya kufundisha mazuwaru wa Imamu Ali (a.s) usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu

Maoni katika picha
Maahadi ya Qur’ani tukufu katika mkoa wa Najafu, chini ya Majmaa ya Qur’ani tukufu katika Atabatu Abbasiyya, imefungua vituo vya kufundisha mazuwaru wanaoenda katika malalo ya kiongozi wa waumini (a.s) kumpa pole katika kumbukumbu ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), usomaji sahihi wa Qur’ani tukufu kwa ushiriki wa walimu (20) wa Qur’ani.

Vituo vinajukumu la kufundisha usomaji sahihi wa surat Faat-ha na sura fupifupi pamoja na nyeradi za swala, sambamba na kujibu maswali na kutoa ufafanuzi wa Qur’ani na kugawa folda zenye mafunzo ya ziara na mambo yanayohusu Qur’ani, vituo hivyo vimefunguliwa kwenye barabara zinazotumiwa na mazuwaru, tawi la Maahadi ya Qur’ani limekua likifanya hivyo kwa miaka mingi, ratiba hiyo ni sehemu ya muendelezo wa ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), zaidi ya watu elfu (11) wamenufaika na ratiba hiyo.

Vituo vimepata muitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru, hasa kundi la vijana ambao hawajamaliza masomo, na wazee ambao hawawezi kusoma kwa usahihi, na hao ndio walengwa wakuu wa mradi huu, hakika kusihi kwa swama kunategemea usomaji sahihi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: