Idara ya waliopotelewa katika Atabatu Abbasiyya imetoa wito kwa mazuwaru waje kuchukua vitu walivyo poteza

Maoni katika picha
Idara ya waliopotelewa katika Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kitengo cha zawadi na nadhiri, imetoa wito kwa mazuwaru waliotembelea malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wakati wa ziara ya Arubaini na kupoteza vitu vyao, wawajulishe kupitia njia zifuatazo:

  • - Wafike kwenye ofisi za idara zilizopo katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) karibu na mlango wa Alqami.
  • - Waangalie kwenye ukurasa wa idara uliopo katika mtandao wa Alkafeel kupitia link ifuatayo: https://alkafeel.net/lost/.
  • - Watuandikie barua pepe kwa anuani ifuatayo: lost@alkafeel.net.
  • - Watupigie simu kwa namba ifuatayo: (009647804947331).
  • - Waangalie ukuraza wa idara kwenye facebook.

Idara imesha fanikiwa kurudisha makumi ya vitu mbalimbali vilivyopotezwa na mazuwaru kwa wenye navyo, vilivyo okotwa ndani ya Ataba na maeneo Jirani, kitu chochote kinacho okotwa huandikwa kwenye orodha maalum halafu hutunzwa kulingana na aina ya kitu hicho, ili mwenye nacho aje kukitambua na kukichukua.

Kumbuka kuwa mtandao wa kimataifa Alkafeel umeandaa ukurasa maalum wa watu waliopotelewa kupitia link ifuatayo (alkafeel.net/lost), hutoa nafasi kwa mazuwaru ya kuja kuangalia mali zao walizo poteza katika Atabatu Abbasiyya tukufu au maeneo jirani, na hurudishiwa baada ya utambuzi, sawa iwe ni kito cha thamani, pesa, beji, simu, kamera au kitu kingine chochote, au vitambulisho kama (kitambulisho cha taifa, paspoti, kitambulisho cha kazi na vinginevyo).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: