Miongoni mwa mfululizo wa vita vya kitamaduni: ni toleo la kitabu cha (facebook ya taifa ni mbadala kwa vijana)

Maoni katika picha
Hivi karibuni kituo cha tafiti za kiislamu na masomo ya kimkakati chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetoa kitabu cha (facebook ya taifa ni mbadala kwa vijana) cha muandishi na mtafiti Ali Lufta Al-Isawi.

Hili ni miongoni mwa matoleo mapya yanayochapishwa na kituo, yanayo lenga kupambana na taasisi kubwa pamoja na miradi inayolenga kuharibu umma wa kiislamu, na kuondoa utambulisho wake wa Dini kwa njia ya moja kwa moja au nyuma ya pazia kupitia madai ya uongo, kwa mfano: kazi, lugha, maendeleo, uvumilivu, utamaduni, uzalendo na madai mengine mengi yanayo haribu umma na kubadilisha utambulisho na utamaduni wake.

Utafiti umefanywa chini ya anuani isemayo (facebook: ni taifa mbadala kwa vijana), ni sehemu ya utafiti unaopambana na utandawazi, katika jamii yetu ya kiislamu, mitandao ya mawasiliano ya kijamii inasababisha mabadiliko makubwa katika Maisha ya watu na tamaduni zao, hususan kizazi kipya cha vijana wa sasa.

Mtandao wa (facebook) ni maarufu sana duniani, unatumiwa na watu wengi zaidi, utafiti huu umejaribu kuangalia athari inayopatikana kwa vijana kutokana na -kutumia mtandao wa facebook- na jinsi wanavyo uchukulia mtandao huo, ambao ni chanzo kikubwa cha utumiaji wa vilevi, kuasi sheria za Dini, misingi ya jamii na kufeli kwenye masomo, sambamba na kuiga tabia mbaya.

Kituo kimebainisha kuwa: sisi tunatoa kazi hii kwa lengo la kuamsha kalamu zetu katika hauza na vyuo, ili ziandike na kuonyesha hazina ya turathi za kiislamu na kuziwasilisha kwa kizazi kipya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: