Muhimu: Atabatu Abbasiyya tukufu imekanusha kuunga mkono upande wowote katika uchaguzi

Maoni katika picha
Baadhi ya vyombo vya habari visivyokuwa makini katika kutafuta habari sahihi za kutangaza kwenye luninga zake au mitandao ya kujamii, vimetangaza kuwa Atabatu Abbasiyya imeunga mkono upande maalum kwenye uchaguzi huu.

Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya unasisitiza kuwa habari hiyo sio ya kweli, na watavishtaki vyombo hivyo vilivyo vunja kanuni za utangazaji kwa mujibu wa sheria.

Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa wito kwa vyombo vyote vya habari kuwa makini vinapotoa taarifa, viwasiliane na wasemaji ramsi wa taasisi wanazotaka kuziripoti ili vipate taarifa sahihi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: