Chuo kikuu Al-Ameed kinapokea wanafunzi na kimetangaza kuanza mwaka mpya wa masomo

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu leo siku ya Jumanne, kimeanza kupokea wanafunzi wapya wa kitivo cha (udaktari, udaktari wa meno, famasia na uuguzi) katika hatua zote za masomo, kimetangaza kuanza mwaka mpya wa masomo (2021 – 2022), chini ya utekelezaji mkali wa kanuni za usafi na kujikinga na maambukizi, kama ilivyo elekezwa na wizara ya elimu ya juu na tafiti za kielimu.

Katika mapokezi ya wanafunzi alikuwepo pia rais wa chuo Dokta Muayyad Ghazali na wasaidizi wake, rais wa chuo ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Maandalizi ya mwaka huu yalianza mapema, kuweka mazingira mazuri ya masomo, tumesha kamilisha maandalizi katika kila kitu cha lazima katika kupokea wanafunzi kwenye vitivo vyote vya chuo, tumeandaa kumbi za masomo na kuweka vifaa vya afya, sambamba na kuandaa ratiba za mihadhara ya masomo na mengineyo, ili kuhakikisha mwaka wa masomo unakua wenye mafanikio na kufikia malengo tarajiwa, tumehitimisha maandalizi kwa kuanza kupokea wanafunzi wetu watukufu”.

Akaongeza kuwa: “Tunatarajia mwaka huu uwe tofauti, uendeleze mafanikio ya chuo, kutokana na juhudi za watumishi na uwepo wa vifaa vyote muhimu, pamoja na jitihada za wanafunzi zitakazo wafanya wawe na maendeleo mazuri”.

Akabainisha kuwa: “Tumesisitiza wanafunzi na watumishi wafuate maelekezo ya wizara, kuhusu namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, na kupata chanjo ya Korona ili kuwa na mazingira salama kiafya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: