Mawakibu za kuomboleza zikiwa mbele ya malalo mbili takatifu zinasema Mwenyezi Mungu akuze malopo yako ewe Imamu wa zama

Maoni katika picha
Kwa maneno ya huzuni ya kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na Imamu wa zama (a.f), waombolezaji wa kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s) ambacho kumbukumbu yake inasadifu leo siku ya Ijumaa mwezi nane Rabiul-Awwal.

Tangu asubuhi mawakibu za kuomboleza za Karbala zimekuja katika malalo mbili takatifu kutoa pole ya msiba huu mkubwa, chini ya ratiba iliyopangwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili takatifu, matembezi ya mawakibu hizo yalianzia katika maeneo yao na kuelekea katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ambako wametoa pole na kuomboleza ndani ya haram yake tukufu, kisha wakaelekea katika malalo ya bwana wa mashahidi (a.s), wakapita kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili huku wanapiga matam na kuhuzunika kwa msiba huu, wakahitimisha matembezi yao katika haram ya bwana wa mashahidi Abu Abdillahi Hussein (a.s).

Tambua kuwa mawakibu za kuomboleza katika mji mtukufu wa Karbala, zimezowea kufanya matembezi ya uombolezaji katika kila tukio la huzuni linalohusu watu wa nyumba ya Mtume (a.s), kwenda kumpa pole bwana wa mashahidi Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuhuisha utiifu kwao na kwa Imamu Mahadi msubiriwa (a.f).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: