Mazuwaru wanaomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s) mbele ya malalo yake huko Samaraa

Maoni katika picha
Kwa nyoyo zilizojaa huzuni na macho yanayotoka machozi mazuwaru wanaomboleza kifo cha Imamu Hassan Askariy (a.s) mbele ya malalo yake takatifu katika mji wa Samaraa, wameanza kumiminika sehemu hiyo takatifu kwa zaidi ya siku tatu, na kilele chake kilikua Adhuhuri ya leo, wanakumbuka kifo cha Imamu aliyeuawa kwa sumu na kumpa pole Imamu wa zama (a.f) kwa msiba huu mkubwa, unaohuzunisha nafsi za Maimamu wa Ahlulbait (a.s) na wapenzi wao katika siku kama hii, mwezi nane Rabiul-Awwal mwaka wa (260) hijiriyya, alikufa kwa sumu aliyopewa na mtawala wa Abbasiyya wa wakati huo, aitwae Mu’tamadi Abbasi.

Atabatu Abbasiyya tukufu na watumishi wake wamefanya kila wawezalo katika kuhudumia mazuwaru na mawakibu za kuomboleza, zinazoenda katika ardhi hiyo takatifu, kwa ajili ya kutoa pole na kuomboleza msiba huo, ili kuwawezesha kufanya ibada ya ziara kwa amani na utulivu, kuna mawakibu nyingi za kutoa huduma, zaairu anapewa kila anacho hitaji kama vile chakula, vinywaji, huduma za matibabu na zinginezo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: