Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa chancho ya Korona kwa watumishi wake

Maoni katika picha
Idara ya madaktari katika Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa chacho ya Korona kwa watumishi wake, kwa lengo la kupunguza maambukizi ya virusi hivyo na kulinda usalama wao pamoja na kuweka mazingira salama kiafya.

Kiongozi wa idara Dokta Osama Abdulhassan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Chanjo inatolewa kwa kushirikiana na idara ya afya ya mkoa wa Karbala, nayo ni sehemu ya juhudi za Atabatu Abbasiyya za kupambana na janga la Korona, na kulinda usalama wa afya za watumishi na mazuwaru, kiasi kikubwa cha chanjo kimeandaliwa, kila mtumishi aliyekua bado hajachanjwa, anaweza kuchanjwa hivi sasa chini ya utaratibu uliowekwa na wizara ya afya”.

Akafafanua kuwa: “Chanjo imepatikana kwa kushirikiana na idara ya afya ya mkoa wa Karbala, wameandaliwa wahudumu maalum wa mambo ya chanjo, pamoja na kuandaa vifaa vyote hitajika katika utoaji wa chanjo chini ya kanuni za wizara ya afya, chanjo zitatolewa kila siku hadi watumishi wote wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanaopenda kuchanjwa watakapo isha”.

Akamaliza kwa kusema: “Kuchanja Korona limekua jambo la lazima kutokana na mazingira tunayo ishi, inasaidia kujilinda na awamu nyingine itakayokuja -Allah atuepushie-, pia inasaidia kupunguza maambukizi ya Korona, hakika chanjo ni kinga ya maambukizi, inalinda afya ya muili na kuzuwia kusambaa kwa virusi”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya kila iwezalo katika kulinda afya za watumishi wake, kwa kusaidia usambazaji wa chanjo ya Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: