Muda na ratiba ya kongamano la kimataifa Daru Rasuulul-A’dham (s.a.w.w) awamu ya pili

Maoni katika picha
Daru Rasuulul-A’dham (s.a.w.w) chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza ratiba ya kongamano la kimataifa awamu ya pili, litakalo fanyika mwezi (14 – 15 Rabiul-Awwal 1443h) sawa na tarehe (21 – 22 Oktoba 2021m) chini ya kauli mbiu isemayo: (Mtume kutoka kwa Mwenyezi Mungu anasoma nyaraka takatifu) na anuani isemayo: (Historia ya Mtume katika Qur’ani na riwaya sahihi).

Kamati ya maandalizi imesema kuwa kongamano litaanza asubuhi ya Alkhamisi tarehe (21 Oktoba) saa tatu, ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na litaendelea kwa muda wa siku mbili, Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi atahutubia kikao cha ufunguzi, aidha kutakua na hutuba zingine pia, kisha zitaendelea kuwasilishwa mada za kitafiti kutoka kwa wahadhiri wa ndani na nje ya Iraq, kwa mujibu wa mada maalum za kongamano zifuatazo:

Mada ya kwaza: Historia ya Mtume mtukufu kabla ya utume katika Qur’ani na riwaya sahihi.

Mada ya pili: Historia ya Mtume mtukufu baada ya utume katika Qur’ani na riwaya sahihi.

Mada ya tatu: Vita alivyopigana Mtume (s.a.w.w) na misafara yake ya kivita katika Qur’ani na riwaya sahihi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: